Kuhusu Mwandishi wa TBC kuzongwa/kuzuiliwa kutimiza wajibu wake
Tumepokea kupitia vyombo vya Habari taarifa za tukio la Mwandishi wa habari wa TBC kushindwa kutimiza wajibu wake katika makao makuu ya CHADEMA.
Tunapenda kuweka wazi kuwa tukio hili halikufanywa kwa maelekezo ya kiongozi yeyote na kama Chama htatujawahi na hatuna sera wala msimamo wa kubagua chombo chochote cha habari.
Kwa hatua za awali, tunafanyia uchumguzi tukio hilo ili kuweza kubainisha nini hasa kilitokea katika siku hiyo na tunategemea kupata ushirikiano kutoka kwa mwandishi husika katika uchunguzi wetu.
Tunapenda kuwahakikishia waandishi wote wa habari kuwa wataendelea kuwa salama katika matukio yote ambayo yatakuwa yakifanywa na CHADEMA na watapata ushirikiano unaostahili.
Baada ya uchunguzi wetu kukamilika tutatoa taarifa kamili juu ya tutakachokuwa tumebaini na hatua tutakazozichukua.
Sisi tunaamini katika uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa waandishi na haki ya kupata na kutoa habari/taarifa kuwa nguzo kuu katika kujenga taifa la demokrasia na hatimayea kufikia maendeleo ya kweli.
Imani yetu hiyo tumekuwa tukiidhihirisha kwa vitendo hadharani, mfano CHADEMA ni taasisi ya kwanza ya kisiasa iliyotia saini na kukubaliana na Azimio la Dar es salaam juu ya uhuru wa Uhariri na Uwajibikaji (hatuna uhakika kama ipo nyingine iliyofanya hivyo hadi sasa).
Tunapenda kutumia fursa hii kuwahakikishia wadau wote wa habari wakiwemo waandishi, wahariri na wananchi kuwa tutaendelea kuionesha imani hiyo kwa vitendo katika shughuli zetu zote za kisiasa .
John Mrema,Mkurugenzi wa Itifaki,Mawasiliano na Mambo ya nje-CHADEMA
source:Jamii forum
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MAHUSIANO
DALILI ZINAZOONESHA KUWA UPO KATIKA MAHUSIANO YA KIMAPENZI AMBAYO SIO SAHIHI Sisi sote tunapenda kuwa na furaha pamoja na kupendwa katik...
-
Muda ni umbali wa kifikra uliopo kati ya matukio mawili yanayofuatana. Umbali huu huweza kupimwa kwa kutumia kizio cha sekunde, dakika,...
-
DALILI ZINAZOONESHA KUWA UPO KATIKA MAHUSIANO YA KIMAPENZI AMBAYO SIO SAHIHI Sisi sote tunapenda kuwa na furaha pamoja na kupendwa katik...
-
Jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) limesema limepokea kwa masikitiko taarifa za kufukuzwa kwa waandishi wa habari wa kituo cha Televishe...

No comments:
Post a Comment